Kipengele Kipya
Sasa unaweza kuongeza mfanyakazi na kumpa ruhusa maalum
Owner Dashboard imesasishwa - simamia timu yako moja kwa moja kutoka simu yako.
Soma zaidiBidhaa, mauzo, matumizi na ripoti - vyote sehemu moja. Jua faida yako ya leo bila kuchimba kwenye daftari.
Vipengele
Umezoea kuandika kwenye daftari, kuhesabu kwa mkono, na kusahau nani anadaiwa nini. Biashara Rahisi inachukua kazi hiyo.
Ongeza bidhaa, fuatilia stock kwa batch, pokea tahadhari stock ikipungua au dawa zikikaribia kwisha muda.
Uza kwa kupiga scan, chagua mteja, chagua namna ya malipo - pokea risiti ya PDF papo hapo.
Rekodi matumizi kwa category, hata ya siku zilizopita. Fuatilia huduma unazotoa kwa tarehe.
Faida, hasara, mzunguko wa stock, ulinganisho wa mwezi na mwezi - bila kuhesabu chochote mwenyewe.
Ongeza wafanyakazi, wape ruhusa maalum kwa kila mmoja. Kila mtu anaona kile kinachomhusu tu.
Muhtasari wa haraka wa mauzo, faida, na hali ya stock ya duka lako - unaufungua tu app.
Jinsi inavyofanya kazi
Jina, eneo, na aina ya biashara - dakika mbili.
Piga picha au andika kwa mkono, weka bei na stock.
Kila mauzo yanahesabika kiotomatiki, faida na stock vinasasishwa papo hapo.
Faida ya leo, wiki, mwezi - wazi mfukoni mwako, siku yoyote.
Matangazo
Vipengele vipya, ushauri wa biashara, na taarifa muhimu kwa wamiliki wa maduka.
Kipengele Kipya
Owner Dashboard imesasishwa - simamia timu yako moja kwa moja kutoka simu yako.
Soma zaidiUshauri
Mambo madogo yanayosababisha hasara kubwa - na jinsi ya kuyaepuka.
Soma zaidiTaarifa
Watu wenye computer wanaweza sasa kutumia app bila kupakua chochote.
Soma zaidiMaswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara
Majibu ya maswali ya kawaida kuhusu Biashara Rahisi.
Ndiyo. Biashara Rahisi ni mfumo wa online ili taarifa za duka zibaki sawa kwenye simu, tablet na kompyuta zilizoidhinishwa.
Vifaa vyovyote unavyohitaji. Data inashirikiwa papo hapo kati ya owner na wafanyakazi wote unaowaongeza, kwenye simu, tablet, au kompyuta.
Ndiyo. Kila akaunti ya mfanyakazi ina ruhusa zake - wewe ndiye unayeamua sehemu gani za app anazoweza kuzifikia, mfano kufanya mauzo au kuona ripoti.
Data yako inahifadhiwa kwa usalama na inahifadhi nakala (backup) kiotomatiki. Ni watu unaowaongeza wewe mwenyewe tu kwenye duka lako wanaoweza kuifikia.
Kuanza ni bure. Fungua duka lako na ujaribu vipengele vya msingi kabla ya kuamua mpango wa malipo.