Kwa maduka, maduka ya dawa na huduma

Duka lako, wazi mfukoni mwako.

Bidhaa, mauzo, matumizi na ripoti - vyote sehemu moja. Jua faida yako ya leo bila kuchimba kwenye daftari.

Data salama kwenye cloud Vifaa vingi, duka moja Ripoti za papo hapo
Duka la AminaLeo, 7 Nov
A
Mauzo LeoTsh 284,500
Bidhaa128 aina
FaidaTsh 61,200
Huduma6 leo
RipotiOna zote
Mauzo (POS)Bidhaa na StockMatumiziHudumaRipotiWatumiaji na RuhusaMauzo (POS)Bidhaa na StockMatumiziHudumaRipotiWatumiaji na Ruhusa

Vipengele

Kila sehemu ya duka lako, sehemu moja

Umezoea kuandika kwenye daftari, kuhesabu kwa mkono, na kusahau nani anadaiwa nini. Biashara Rahisi inachukua kazi hiyo.

Bidhaa na Stock

Ongeza bidhaa, fuatilia stock kwa batch, pokea tahadhari stock ikipungua au dawa zikikaribia kwisha muda.

Mauzo (POS)

Uza kwa kupiga scan, chagua mteja, chagua namna ya malipo - pokea risiti ya PDF papo hapo.

Matumizi na Huduma

Rekodi matumizi kwa category, hata ya siku zilizopita. Fuatilia huduma unazotoa kwa tarehe.

Ripoti na Analytics

Faida, hasara, mzunguko wa stock, ulinganisho wa mwezi na mwezi - bila kuhesabu chochote mwenyewe.

Watumiaji na Ruhusa

Ongeza wafanyakazi, wape ruhusa maalum kwa kila mmoja. Kila mtu anaona kile kinachomhusu tu.

Dashibodi ya Owner

Muhtasari wa haraka wa mauzo, faida, na hali ya stock ya duka lako - unaufungua tu app.

Jinsi inavyofanya kazi

Kuanzia leo, hatua nne

1

Sajili duka lako

Jina, eneo, na aina ya biashara - dakika mbili.

2

Ongeza bidhaa zako

Piga picha au andika kwa mkono, weka bei na stock.

3

Anza kuuza

Kila mauzo yanahesabika kiotomatiki, faida na stock vinasasishwa papo hapo.

4

Ona ripoti yako

Faida ya leo, wiki, mwezi - wazi mfukoni mwako, siku yoyote.

Matangazo

Habari na masasisho ya hivi karibuni

Vipengele vipya, ushauri wa biashara, na taarifa muhimu kwa wamiliki wa maduka.

Kipengele Kipya

Sasa unaweza kuongeza mfanyakazi na kumpa ruhusa maalum

Owner Dashboard imesasishwa - simamia timu yako moja kwa moja kutoka simu yako.

Soma zaidi

Ushauri

Njia 3 za kupunguza hasara ya stock dukani

Mambo madogo yanayosababisha hasara kubwa - na jinsi ya kuyaepuka.

Soma zaidi

Taarifa

Biashara Rahisi sasa inapatikana kwenye Web

Watu wenye computer wanaweza sasa kutumia app bila kupakua chochote.

Soma zaidi

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Bado una swali?

Majibu ya maswali ya kawaida kuhusu Biashara Rahisi.

Ndiyo. Biashara Rahisi ni mfumo wa online ili taarifa za duka zibaki sawa kwenye simu, tablet na kompyuta zilizoidhinishwa.

Vifaa vyovyote unavyohitaji. Data inashirikiwa papo hapo kati ya owner na wafanyakazi wote unaowaongeza, kwenye simu, tablet, au kompyuta.

Ndiyo. Kila akaunti ya mfanyakazi ina ruhusa zake - wewe ndiye unayeamua sehemu gani za app anazoweza kuzifikia, mfano kufanya mauzo au kuona ripoti.

Data yako inahifadhiwa kwa usalama na inahifadhi nakala (backup) kiotomatiki. Ni watu unaowaongeza wewe mwenyewe tu kwenye duka lako wanaoweza kuifikia.

Kuanza ni bure. Fungua duka lako na ujaribu vipengele vya msingi kabla ya kuamua mpango wa malipo.

Ona maswali yote →

Acha daftari. Fungua duka lako kidijitali leo.

Bure kuanza. Hakuna kadi ya benki inayohitajika.

Anza sasa
💬